Luke 5:1-6

Kuitwa Kwa Wanafunzi Wa Kwanza

(Mathayo 4:18-22; Marko 1:16-20)

1 aSiku moja Isa alipokuwa amesimama karibu na Ziwa la Genesareti,
Yaani Bahari ya Galilaya.
watu wengi wakiwa wanasongana kumzunguka ili wapate kusikia neno la Mungu,
2akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa, zikiwa zimeachwa hapo na wavuvi waliokuwa wanaosha nyavu zao. 3 cAkaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba aisogeze ndani ya maji kidogo kutoka ufuoni. Kisha akaketi na kufundisha watu akiwa mle ndani ya mashua.

4 dAlipomaliza kunena, akamwambia Simoni, “Sasa peleka mashua hadi kilindini kisha mshushe nyavu zenu mkavue samaki.”

5 eSimoni akamjibu, “Bwana, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha na hatukuvua chochote. Lakini, kwa neno lako nitazishusha nyavu.”

6 fNao walipozishusha nyavu zao, wakavua samaki wengi sana, nyavu zao zikajaa zikaanza kukatika.
Copyright information for SwhKC